1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yafanya shambulizi jipya dhidi ya waasi Yemen

13 Januari 2024

Marekani imefanya Jumamosi shambulizi jipya dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen. Hii ni baada ya wapiganaji hao wanaoungwa mkono na Iran kuonya dhidi ya mashambulizi zaidi kwenye meli zinazotumia Bahari ya Shamu

https://p.dw.com/p/4bCnX
Nahostkonflikt Jemen | Militärschlag gegen Huthi-Rebellen
Picha: US Central Command via X/REUTERS

Marekani imefanya shambulizi jipya dhidi ya eneo la waasi wa Houthi nchini Yemen. Hii ni baada ya wapiganaji hao wanaoungwa mkono na Iran kuonya dhidi ya mashambulizi zaidi kwenye meli zinazotumia Bahari ya Shamu.

Soma pia:Marekani na Uingereza zashambulia ngome za wahouthi, Yemen

Shambulizi hilo kwenye eneo lililo na rada ya Wahouthi limefanyika siku moja baada ya wanajeshi wa Marekani na Uingereza kuyapiga maeneo kadhaa ya Yemen, na kuongeza hofu kuwa vita vya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas vinaweza kusambaa hadi kanda nzima. Wahouthi wanawaunga mkono Wapalestina katika vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, Israel imeendelea kuyalipua maeneo ya Gaza wakati vita hivyo vikifikisha siku mia moja hapo kesho. Makombora ya Israel yalidondoshwa katika maeneo kati ya miji ya kusini ya Khan Younis na Rafah. Wizara ya afya ya Gaza inayomilikiwa na Hamas imesema watu 60 waliuawa jana usiku katika mashambulizi ya Israel kwenye ukanda huo ambao pia unakumbwa na ukosefu wa mawasiliano ya simu na intaneti.