1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani yafanya mashambulizi ya anga huko Iraq na Syria

3 Februari 2024

Jeshi la Marekani jana limefanya mashambulizi ya anga na kuvilenga zaidi ya vituo 85 vinavyohusiana na jeshi la wanamapinduzi la Iran na wanamgambo inaowaunga mkono nchini Iraq na Syria.

https://p.dw.com/p/4c0JL
Marekani | Iraq | Syria
Mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya vituo vya Iran huko Iraq na SyriaPicha: picture alliance/Anadolu

Jeshi la Marekani jana limefanya mashambulizi ya anga na kulenga zaidi ya vituo 85 vinavyohusiana na jeshi la wanamapinduzi la Iranna wanamgambo inaowaunga mkono nchini Iraq na Syria.

Mashambulizi hayo ni hatua za ulipaji kisasi wa shambulizi la wiki iliyopita lililofanyika nchini Jordan na kuwaua wanajeshi watatu wa Marekani.

Mashambulizi ya jana Ijumaa ambayo yalihusisha matumizi ya mabomu ya masafa marefu ya B-1, ni ya kwanza katika hatua kadhaa za utawala wa Rais Joe Biden, kujibu shambulizi la wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

Wakati mashambulizi hayo hayakulenga maeneo ndani ya Iran, lakini yanaashiria kuongezeka kwa mvutano huko Mashariki ya Kati ambako bado kunashuhudiwa vita vya takribani miezi minne baina ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.