SiasaMarekani
Marekani yaanza kuondoa wanajeshi wake nchini Niger
19 Mei 2024Matangazo
Tangazo la kuanza kuondoka wanajeshi hao limetolewa kwa pamoja na nchi hizo mbili mapema hii leo.
Taarifa hiyo imesema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kabla ya Septemba 15. Pande hizo zilitangaza kufikia makubaliano ya kuondolewa wanajeshi hao waliopelekwa kuisaidia Niger kupambana na makundi ya itikadi kali za dini.
Utawala mpya wa kijeshi ulioipindua serikali ya kidemokrasia katikati mwa mwaka jana ulisema wanajeshi hao wa Marekani walikuwemo nchini Niger kinyume cha sheria.
Kwa jumla Marekani inao askari 650 nchini Niger pamoja na kambi kubwa ya droni karibu na mji wa kaskazini mwa taifa hilo wa Agadez.