Marekani, UK zaahidi jibu la haraka kwa maombi ya Ukraine
12 Septemba 2024Marekani na Uingereza zimeahidi jana Jumatano, kupitia haraka maombi ya Ukraine kuelgeza vizuwizi juu ya matumizi ya silaha za mataifa hayo kushambulia ndani ya Urusi, huku zikiahidi msaada mpya wa dola bilioni 1.5, kabla ya msimu mgumu wa baridi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake mpya wa Uingereza David Lammy, waliizuru Kyiv baada ya kufanya safari ya masaa tisa kwa njia ya treni wakitokea Poland.
Soma piaUS, UK kutafakari ombi la Kyiv kulegeza vikwazo vya kutumia silaha zao ndani ya Urusi:
Ziara hiyo ilijiri wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu hali katika uwanja wa kivita, na mashaka juu ya msimamo wa baadae wa Marekani kuhusu vita hivyo.
Blinken alisema atawasilisha maombi ya Ukraine kwa rais Joe Biden, na kuongeza kuwa Biden na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, watazungumzia suala hilo watakapokutana Ijumaa hii mjini Washington.