1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na wakuu wa mataifa mengine wamelaani kuuawa kwa ki

18 Septemba 2024

Marekani na wakuu wa mataifa mengine wamelaani kuuawa kwa kiongozi mwingine wa harakati za mazingira nchini Honduras na kusema kifo hicho kinaongeza wasiwasi wa mauaji ya wanaharakati hao huko Amerika ya Kusini.

https://p.dw.com/p/4kjrC
Mwanaharakati wa Honduras Juan Lopez
Mwanaharakati wa mazingira aliyekuwa akipinga uchimbaji madini ili kulinda mazingira Juan López ameuawaPicha: Orlando Sierra/AFP

Rais wa Honduras Xiomara Castro alithibitsia kifo cha Juan López siku ya Jumamosi katika eneo la Colon, kuliko na idadi kubwa ya wanaharakati wanaopinga miradi ya uchimbaji wameuawa.

López alipigwa risasi katika manispaa ya Tocoa baada ya miaka kadhaa ya kupinga makampuni ya uchimbaji ili kulinda mito na misitu ya eneo hilo, limesema shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetaka uchunguzi na kulaani vikali mauaji hayo. Umoja wa Mataifa nao umetoa kauli kama hiyo na kutaka wahusika kuwajibishwa.