Marekani na Saudi Arabia zashtumu kurejea kwa vita Sudan
12 Juni 2023Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, Marekani na Saudi Arabia zilisema Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) waliweza kudhibiti vikosi vyao wakati wa muda huo lakini mataifa hayo mawili yamesononeshwa sana na hali ya kuanza kwa vurugu kali mara moja. Mapigano makali yameikumba Sudan tangu katikati ya Aprili, baada ya mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, anayeongoza kikosi cha RSF, kuanza kuzozana.