1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Marekani, Korea Kusini kukabiliana na kitisho cha Pyongyang

27 Aprili 2023

Rais Joe Biden wa Marekani na mgeni wake, Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini, wamezungumza juu ya kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuzuia kitisho kinachoongezeka kutokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4Qbsn
Südkoreas US-Militär
Picha: Chung Sung-Jun/Pool Photo/AP/picture alliance

Viongozi hao wanakutana huku kukiwa na ongezeko la vitisho kutoka kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wakati ambapo nchi yake inaongeza uwezo wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kufika Marekani.

Soma zaidi:Marekani na washirika wake wafanya mazoezi ya kijeshi

Wakati huo huo Marekani imetangaza kuwa itapeleka nyambizi yenye uwezo wa kufyatua makombora ya nyuklia nchini Korea Kusini kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Marais Biden na Yoon pia wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki, magari ya umeme na betri.