1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na Korea Kusini kufanya luteka

3 Machi 2023

Marekani na Korea Kusini zitafanya luteka ya pamoja ya kijeshi ya siku 10, kuanzia Machi 13 hadi 23.

https://p.dw.com/p/4OCVP
Südkorea Militär-Übung
Picha: South Korean Defence Ministry/AFP

Maafisa kutoka nchi hizo mbili wamesema leo kuwa luteka hiyo iliyopewa jina ''Ngao ya Uhuru'', inalenga kuimarisha ulinzi na nguvu ya pamoja ya kujihami dhidi ya uchokozi wa Korea Kaskazini.

Mazoezi yaliyopita ya kijeshi yaliibua hisia kali kutoka kwa Korea Kaskazini, ambayo imekuwa ikurusha makombora ya masafa marefu pamoja na kutoa vitisho vya kutumia silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini imesema luteka kama hiyo ni ushahidi kwamba Marekani na washirika wake wanajiandaa na vita vya uchokozi.

Jeshi la Marekani limeionya Korea Kaskazini kwamba matumizi ya silaha za nyuklia yatasababisha mwisho wa utawala wa nchi hiyo.