1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuimarisha ushirikiano na washirika

10 Oktoba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameelezea matumaini ya kuimarisha ushirikiano na Thailand, walipokutana na waziri mkuu mpya wa Thailand.

https://p.dw.com/p/4le0q
ASEAN Gipfel
Picha: Tang Chhin Sothy/AP/picture alliance

Viongozi hao wamekutana katika mkutano wa kilele wa Asia kufuatia msukosuko wa hivi karibuni nchini Thailand.

Blinken amekutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, mrithi wa himaya ya kisiasa ambaye alichukua hatamu za uongozi mwezi mmoja uliopita baada ya mtangulizi wake kuondolewa madarakani na chama kikuu cha upinzani kuvunjwa.

Katika mazungumzo yao Blinken amesema Marekani inatarajia kushirikiana na Thailand katika kuzingatia mambo ambayo yataboresha maisha, ikiwa ni pamoja na uchumi, usalama na mabadiliko ya hali ya hewa.

Blinken anaiwakilisha Marekani katika mkutano wa kila mwaka wa mataifa ya ASEAN, ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.