1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani kuendeleza mazungumzo ya mzozo wa Sudan

13 Agosti 2024

Marekani inasisitiza kwamba itaendelea na kuanzisha mazungumzo ya kusitisha mapigano ya Sudan wiki hii, hata ikiwa serikali ya Sudan haitohudhuria.

https://p.dw.com/p/4jP8U
Abdul Fattah Al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo
Viongozi hasimu wa Sudan Abdul Fattah Al-Burhan na Mohamed Hamdan DagaloPicha: Bandar Algaloud/Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Marekani inasisitiza kwamba itaendelea na kuanzishamazungumzo ya kusitisha mapigano ya Sudan wiki hii, hata ikiwa serikali ya Sudan haitohudhuria. Mazungumzo hayo yatafanyika katika eneo ambalo halijawekwa wazi nchini Uswisi na yanatarajiwa kuanza Jumatano na huenda yakadumu kwa siku kumi.

Wakati kundi la wanamgambo wa RSF likiwa limekubali mwaliko, serikali ya Sudan imeonesha kutoridhishwa na mwelekeo itakaochukua Marekani katika mazungumzo hayo na haijathibitisha iwapo ina nia ya kuhudhuria. Mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan, Tom Porriello, amesema wamekuwa na mazungumzo ya kina na jeshi la Sudan ila halijatoa ishara ya kuhudhuria. Porriello anadai watajikita tu katika masuala ya kimataifa na kiufundi ila jeshi la Sudan litakapothibitisha kuhudhuria, basi wataangazia suala la upatanishi katika mazungumzo yao.