1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani Japan na Australia zapanga luteka ya pamoja

20 Agosti 2023

Maafisa wa Usalama wa Ufilipino wamesema Marekani, Japan na Australia wanapanga kufanya luteka ya pamoja ya jeshi la wanamaji katika Bahari ya Kusini mwa China, upande wa Magharibi mwa Ufilipino wiki hii.

https://p.dw.com/p/4VN1X
USS Nimitz Drill Südchinesisches Meer
Picha: ABACA/picture alliance

Hatua hiyo inaonyesha kujitolea kwao kuheshimu utawala wa kisheria katika kanda hiyo, baada ya kisa cha hivi karibuni cha uchokozi wa China katika bahari hiyo inayozozaniwa.  

Luteka hiyo itajumuisha ndege tatu pamoja na helikopta zitakazoendeshwa kwa pamoja kuonyesha nguvu zao. Makamanda wa pande zote wanatarajiwa kukutana na wenzano wa Ufilipino baada ya luteka hiyo. 

Marekani na Ufilipino waungana kiulinzi wakati uchokozi wa China ukiongezeka

Tarehe tano mwezi huu, meli za walinzi wa pwani wa China zilitumia mizinga ya maji dhidi ya meli za Ufilipino katika bahari hiyo inayogombaniwa ambapo mivutano kwa muda mrefu inachukuliwa kama mambo yanayoweza kuzusha machafuko na imekuwa kiini cha uhasama kati ya Marekani na China katika kanda hiyo.