1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Ni vigumu Ukraine kujiunga na NATO Julai

14 Februari 2024

Balozi wa Marekani katika Jumuiya ya Kujihami NATO amesema hatarajii Ukraine itaalikwa kujiunga na muungano huo Julai.

https://p.dw.com/p/4cMlE
Uswisi | Kongamano la Kiuchumi Duniani huko Davos | Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskiy alipoudhuria mkutano wa 54 wa kila mwaka wa Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswizi, Januari 16, 2024.Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Balozi wa Marekani katika Jumuiya ya Kujihami NATO amesema hatarajii Ukraine itaalikwa kujiunga na muungano huo katika mkutano wa Julai licha ya ombi lake la dharura la uanachama kufuatia uvamizi wa Urusi. Smith amesema anaamini mkutano huo wa mwaka huu wa mjini Washington utaonesha nia ya kujisogeza zaidi kwa Ukraine na kwamba utachukua hatua madhubuti kutumika kama daraja kati ya walipo sasa na uanachama kamili. Mwaka jana mataifa wanachama wa NATO yalisisitiza msimamo wa muda mrefu kwamba serikali ya Kyiv siku moja itakuwa mwanachama wa muungano wa kijeshi unaoongozwa naMarekani, lakini hazikuweka wazi muda.