1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

maradhi ya Marburg yaangamiza maisha nchini Angola

12 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNp

Luanda

Watu zaidi ya 200 wamekufa kutokana na maradhi ya kuambukiza ya Marburg nchini Angola.Pekee katika mkoa wa Uige watu wasiopungua 184 wanasemekana wamefaeriki dunia-hayo ni kwa mujibu wa ripoti za wizara ya afya ya Angola na shirika la afya la kimataifa WHO.Kati ya wagonjwa 221,2003 wamefariki dunia,ripoti hizo zimesema.Kwa mujibu wa wataalam,vijidudu vya Marburg vinatapakaa na kuambukiza kutokana na mate,jasho na maji maji mengineyo ya mwili.Hakuna bado chanjo kujikinga na maradhi hayo.