1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Maporomoko ya udongo yauwa 100 Papua New Guinea

24 Mei 2024

Televisheni ya taifa ya Papua New Guinea imetangaza kuwa zaidi ya watu 100 wanahofiwa kufariki dunia nchini humo kutokana na maporomoko ya udongo.

https://p.dw.com/p/4gETY
Maporomoko ya udongo yameuwa zaidi ya watu 100 nchini Papua New Guinea.
Maporomoko ya udongo yameuwa zaidi ya watu 100 nchini Papua New Guinea.Picha: Ninga Role/AAP/IMAGO

Kwa mujibu wa kituo hicho cha televisheni,  maporomoko hayo yametokea mapema katika kijiji cha Kaokalam kwenye mkoa wa Enga ulio umbali wa takribani kilomita 600 kaskazini magharibi ya mji mkuu, Port Moresby.

Soma zaidi:Marape: Papua New Guinea haina makubaliano ya usalama na China 

Ingawa maafisa hawajathibitisha idadi kamili ya vifo, shirika la habari la nchini humo, JB143, limeandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba maporomoko hayo yamefunika majumba, mashamba na idadi isiyojulikana ya watu.