Mapigano yazuka tena Sudan
22 Aprili 2023Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Ujerumani DPA katika eneo la tukio amesema katika mji mkuu wa Khartoum kumetokea miripuko mingine ya mabomu, huku mashuhuda wengine wakiandika katika kurasa zao za Twittr kusikika kwa milio ya risasi.
Mwandishi DPA alisema usitishwaji mapigano uliokuwa na lengo la kutoa nafasi ya sherehe za Eid al-Fitr kwa kuadhimisha mwisho Mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa kiasi kikubwa ulifanyika wakati wa usiku ingawa pia kulikuwa na kile alichosema mapigano ya hapa na pale.
Mapigano nchini Sudan yalizuka takribani juma moja lililopita kati ya majenerali wawili wenye nguvu zaidi na vitengo vyao vya kijeshi. Kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan, ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi, anakabliana na naibu wake Mohammed Hamdan Dagalo, kiongozi kikundi chnye nguvu cha kijeshi cha RSF.