"Mapigano yasitishwe Congo"
21 Novemba 2012Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa Dw aliyekuwepo mjini New York baraza hilo limepanga kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo la M23 sambamba wanaowasaidia kutoka nje ya DRC. Hata hivyo hawakufafanmua zaidi kuhusu wasaidizi hao.
Aidha baraza hilo limemuomba katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon atoe mapendekezo yake kwa baraza hilo ya namna ya kufanikisha kumalizika kwa mzozo katika eneo la Kivu.
Nguvu za kijeshi ziongezwe
Sambamba na hilo limesema kuna umuhimu wa kukiongezea nguvu zaidi kikosi cha umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO ili kiweze kujihami pamoja na kuwalinda raia.
Pamoja na mambo mengine katika mapendekezo yake kwa baraza la usalama serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilitaka kuwepo kwa aufafanuzi zaidi kuhusi kwa rwanda katika machafuko hayo ya mashariki mwa Congo.
Rwanda yaendelea kujitetetea
Kwa mujibu wa afisa mwandamzi wa Rwanda katika umoja wa Mataifa, Olivier Nduguhungirehe aliendelea kukana kuhusika kwa taifa lake na kundi la waasi wa M23. Hata hivyo afisa huyoamesema kiniachoweza kumaliza machafuko hayo ni mazungumzo kati ya waasi na serikali ya Congo.
Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenyewe hali mjini Goma inaelezwa kuwa mbaya zaidi huku idadi kubwa ya wananchi wakiwa katika hofu ya usalama wao, wafungwa waliyoko magerezani wamefunguliwa. Kupata zaidi juu ya kile kinachoendelea, Sudi Mnette amezungumza na Mratibu wa Jumuiya ya Kiraia, Mustafa Mwiti akiwa Goma. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza kitufe cha alama ya kusikiliza masikioni hapo nchini.
Mwandishi:Amina Abubkar
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman