SiasaSudan
Mapigano yaendelea Sudan licha ya kurejea kwa mazungumzo
30 Oktoba 2023Matangazo
Lakini licha ya kuanza kwa mazungumzo hayo, mapigano hayaonyeshi dalili za kupungua wakati wanapopambana kudhibiti mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Jeshi la anga la Sudan limeshindwa kuwaondoa wapiganaji wa Rapid Support Forces RSF mjini Khartoum kwani bado wanadhibiti mitaa ya mji huo mkuu huku jeshi likiwa na udhibiti wa mashariki mwa nchi.
Katika kipindi cha miezi mitatu sasa RSF imelidhibiti eneo la mpakani la Om Dafouq na wanaripotiwa pia kuchukua udhibiti wa njia za ziada za usambazaji wa bidhaa kuelekea Kahrtoum.
Marekani na Saudi Arabia zinasema mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita yanalenga kuleta makubaliano ya kusitisha mapigano kwa ajili ya kusambazwa kwa misaada ya kiutu.