Mapigano makali yaendelea nchini Sudan
16 Mei 2023Matangazo
Mapigano hayo yamesababisha machafuko katika maeneo mengine ya nchi hiyo, hasa katika mji mkuu Khartoum na katika mkoa wa magharibi wa Darfur.
Katika hatua za hivi karibuni, Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan ameamuru kufungwa akaunti zote za benki za kikosi pinzani cha kijeshi kinachoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.
Milipuko yaendelea Sudan huku vita vikiingia mwezi wa pili
Hadi sasa takriban watu 200,000 wamelazimika kukimbilia nchi jirani huku wengine 700,000 wakiwa wakimbizi wa ndani. Vita hivyo vimezusha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu ambao unatishia pia kuathiri eneo kubwa la ukanda huo.