1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano makali yautikisa mji wa Khartoum nchini Sudan

2 Julai 2023

Mapigano makali kati ya vikosi vya majenerali wanaohasimiana yameutikisa mji mkuu wa Sudan, Khartoum leo Jumapili. Mashuhuda wamesema waliamshwa na mapambano ya silaha pamoja na milio ya ndege za kivita.

https://p.dw.com/p/4TKEK
Sudan | Waffenstillstand General Abdel Fattah al-Burhan
Picha: Sudanese Armed Forces/REUTERS

Mapambano hayo yaliyoanza katikati ya mwezi Aprili mwaka jana kati ya vikosi vya jeshi rasmi la Sudan chini ya Jenerali  Abdel Fattah al Burhan na wapiganaji wa kikosi cha dharura wa RSF yameshasababisha vifo vya karibu watu 3,000. 

Takribani watu milioni 2.2 wamelazimika kuyakimbia makazi yao

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM takribani watu milioni 2.2 wamelazimika kuyakimbia makazi yao huku watu karibu watu 645,000 wakikimbilia kuvuka mipaka ya nchi hiyo kulinda usalama wao kutokana na machafuko nchini humo. Kwa sasa Sudan inakabiliwa pia na magonjwa pamoja na utapia mlo hali inayotishia kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoyahama makazi yao.