1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano makali yaendelea Syria kati ya wapiganaji na jeshi

29 Novemba 2024

Idadi ya vifo kutokana na mapambano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali ya Syria na waasi kaskazini-magharibi wa nchi hiyo imeongezeka na kufikia wapiganaji 182, kwa mujibu wa shirika la ufuatiliaji wa mzozo huo.

https://p.dw.com/p/4nY0t
Mapambano mapya Idlib
Mtoto alijeruhiwa akitibiwa IdlibPicha: Anas Alkharboutli/dpa/picture alliance

Wapiganaji wa kundi la Jihad wamezuwia barabara kuu kati ya Damascus na mkoa wa Alepposiku ya Alhamisi, wakati wa shambulio lililoua takriban watu 200, wakiwemo raia waliolengwa na mashambulizi ya angani ya Urusi.

Kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) na makundi washirika yalianzisha shambulio dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na serikali, na kusababisha mapigano makali zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Soma pia: Mabasi yaanza kuwaondoa raia kutoka vijiji tiifu kwa Syria

Mashambulizi ya anga ya Urusi yaliwaua raia 19, huku HTS na washirika wao wakikata mawasiliano ya barabara kuu ya Damascus-Aleppo ya M5 na kudhibiti makutano ya M4 na M5.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 14,000, nusu yao wakiwa watoto, wamehamishwa kutokana na machafuko hayo.