1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wasikilizaji wa Noa Bongo Jenga Maisha yako

1 Juni 2011

Kutoka nchini Msumbiji hadi Senegal, Burkina Faso hadi Tanzania, wasikilizaji wetu kote barani Afrika wanasema : Sikiliza Ujifunze!

https://p.dw.com/p/RRGP

Ushirikiano wa Learning by Ear’ Noa Bongo Jenga Maisha yako na vituo vya redio shirika 254 kote barani Afrika umeleta muamko mpya na kuwezesha kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi katika kanda hii. Kama ilivyo desturi, tunapenda sana kusikia maoni ya wasikiliazaji wetu na tungependa kuyachapisha hapa.

“Sote tunajifunza kwa kusikiliza. Tunapokwenda shuleni, tunamsikiliza mwalimu. Vivyo hivyo tunasikiliza redio na kujifunza.”
Joaquim Alberto Chissano
Rais wa zamani wa Msumbiji

"Kupitia vipindi vya Learning by Ear, "Noa bongo Jenga Maisha yako" vijana wengi wanapata fursa ya kujifunza mengi mapya kila siku, kama ilivyo shuleni. Redio ni chombo muhimu sana cha mawasiliano kinachoangazia na kusambaza masuala mbalimbali na mawazo."
Youssou N’Dour
Mwanamuziki | Senegal

"Navutiwa sana na vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako. Kwa hakika mnachambua kwa kina mnapofuatilia masuala ya maendeleo katika jamii.Vipindi vyenu vinatumbuiza na kutufunza kwamba sio shuleni pekee mtu anaweza kupata elimu bali jamii pia inaweza kujifunza kupitia redio".
Mourtala Saidon
Msikilizaji| Niger

Nelson Pereira
Nelson Pereira, MsumbijiPicha: DW

"Vipindi vyenu kwa kweli vinasaidia kuelimisha. Binafsi nimejifunza mengi kupitia vipindi mbalimbali."
Nelson Pereira


Mratibu wa Rádio Trans Mundial | Msumbiji

"Kwa maoni yangu vipindi vya Learning by Ear ni wazo zuri sana kwa Afrika - kwa sababu watu hutilia mkazo sana jambo wanalosikia. Na ujumbe husambaa haraka sana kwa maneno."
Félix Koffi Amétépé
Mwandishi wa Habari | Burkina Faso

"Tunawashukuru sana kwa kuanzisha vipindi vya Learning by Ear. Naamini kwa hakika watu wengi wenye mawazo sawa na yangu kuhusiana na ubora wa vipindi hivi, bila shaka watakuwa na mambo mengi ya kusema yanayosisimua kuhusu jinsi vipindi hivi vilivyowasaidia na kuyabadilisha maisha yao."
Kabir Idris Pindiga
Listener | Nigeria

“Napenda kuipongeza Deutsche Welle kwa juhudi zao za kuandaa vipindi murua vya Noa Bongo vinavyolenga kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu ugonjwa hatari wa Ukimwi na HIV, na jinsi ya kujikinga na na magonjwa hayo. Na hakika mvulana au msichana anayesikiliza vipindi hivi anaeleimika vyema kuhusu njia bora za kujikinga.”

Ester Gasau
Msikilizaji | Tanzania

Christine Luzolo
Christine Luzolo, Kongo na UjerumaniPicha: Privat

"Kwenda shule, kujua kusoma na kuandika imekuwa ni bahati kubwa kwangu. Hasa nikifikiria wasichana wengine ambao hawakupata fursa ya kupata elimu mfano bibi yangu, kweli nashindwa kuelezea umuhimu na jinsi nilivyoupenda mchezo wa redio kuhusu elimu."
Christine Luzolo
Msikilizaji | Kongo na Ujerumani

"Vipindi hivi vinatoa habari za kuelimisha na ushauri ambao unapasa kuzingatiwa na wote - sio tu kwa vijana wa leo. Haikutarajiwa."
Gremah Boukar
Mkuu wa kituo cha Redio Amfani | Niger

Sonya Agua
Sonya Agua, RwandaPicha: DW

"Kushiriki kwangu katika kuandaa vipindi hivi vya Learning by Ear kumenipa nafasi ya kupanua tajiriba yangu. Na furahi sana kufahamu nimeweza kusaidia wengine kutokana na mchango wa kazi yangu."
Sonya Agua
Msanii wa Uigizaji | Ruanda

"Napendelea sana kusikiliza mchezo wa redio kuhusu Kompyuta na Intaneti. Nahisi ni kama naanza kujifunza kuhusu teknolojia ya mawasiliano."
Diamantino Maria da Silva
Msikilizaji | Guinea-Bissau

"Sisi tunahusika sana na mapambano ya kitamaduni kwa ajili ya elimu. Na tunatumia redio kuisukuma mbele jamii ya Afrika kupitia msaada kutoka kwa serikali na shirika la utangazaji la Ujerumani la Deutsche Welle."
Sidy Diagne
Mkurugenzi wa kituo cha Redio Dunyya | Senegal