Maoni: Urithi wenye sumu wa Brexit anaoacha Theresa May
7 Juni 2019Katika maoni yake mwandishi wa DW, Rob Mudge anaandika kwamba , msizubaishwe na machozi aliyoyamwaga May wakati akiaga. Waziri mkuu May alipitia katika mchakato wa Brexit ambao umekatikakatika na usiofanya kazi na ameiacha nchi hiyo katika hali inayoshitua ya kama ugonjwa wa kupooza.
Kwa hiyo basi Theresa May anaelekea binafsi katika chochote kile ambacho atajaliwa katika maisha yake ya baada ya waziri mkuu. Hali ya baadaye ya nchi yake , ambayo anajigamba kwamba anaipenda, imo katika hali ngumu zaidi, kama sio katika hali ambayo inaweza kusemwa kwa kebehi, "asante kwa msimamo wake wa mkanganyiko, mtengano na uongo wa Brexit."
Lakini sio tu imani yake ya kufikirika kwa kuamini kwamba anaweza kufanikisha kile alichosema ni "bora kwa nchi yake." Ni vile alivyojaribu kuuza imani hiyo katika Umoja wa Ulaya mjini Brussels na katika baraza la wawakilishi. Wanasema kwamba muonekano unadanganya, lakini alivyokuwa akijitokeza hadharani, ambako kumejitokeza kuashiria kutokuwa na hisia na hali ya wasiwasi, na taswira inayoonesha kila mara kama panya aliyekabiliwa usiku na taa za gari, haikumuonesha kuwa karibu na nchi ambayo imegawika na kuongezeka mtengano.
Kuungama May
Na bila shaka sina imani na mtu ambaye kuungama kwake kufanya kitu cha utundu, eti ni kuwa alikuwa akikimbia katika mashamba ya ngano wakati akiwa mtoto. Katika anguko moja hakukamilisha tu hatma yake lakini bila shaka ile ya vizazi vingine vijavyo kwa tamko lake la "kutopata makubaliano ni bora kuliko makubaliano mabaya." Kwa hiyo, inaonesha kutowajibika kabisa. Katika hali ambayo ni mbaya, jaribio lake la kutumia mamlaka yake ya waziri mkuu kuhalalisha dhana yake hiyo ya uongo, haitasameheka.
Kama Muingereza anayefanya kazi nchini Ujerumani, sina bahati mbaya ya kuamka kila siku na hisia za kudidimia katika nchi ambayo inadidimia. Lakini nilikuwa mjini London kwa ajili ya kura ya kwanza ya wananchi Oktoba mwaka jana, na kushuhudia hasira, kukata tamaa lakini pia dhamira ya mamia kwa maelfu ya watu, vijana na wazee, ambao walikuwa wakipambana kwa amani kujaribu na kuzuwia nchi yao kupotea katika lile tundu, liitwalo tundu jeusi.
May na bila kusahau kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, ambaye anafanana na May katika kuyumbayumba kwao, wamechagua kupuuzia matakwa ya wananchi. Mtazamo wao haukwenda sambamba na ule wa wananchi waliopiga kura mwaka 2016 kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.