1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Putin amepoteza vita vya gesi na Ujerumani

17 Januari 2023

Urusi haiwezi tena kutumia gesi yake asilia kuihilibu Ujerumani. Ujerumani imejaza hifadhi yake bila ya usaidizi wa kampuni ya Urusi Gazprom na imejipanga hadi kipindi kijacho cha baridi, anaandika Andrey Gurkov.

https://p.dw.com/p/4MKNb
Sibirien l Gasförderanlage von Achimgas
Picha: Uwe Zucchi/dpa/picture-alliance

Itakuwa mapema sana kuzungumzia Urusi kushindwa kijeshi katika vita vyake nchini Ukraine. Lakini lile linaloeza kuzungumziwa kwa uhakika ni hatua ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kushindwa katika vita vyake vya gesi dhidi ya Ujerumani. Ujerumani ina hifadhi kubwa ya gesi ndani ya Umoja wa Ulaya, na kama hifadhi hizi zitabakia kuwa ndani ya asilimia 90 ifikapo mwishoni mwa Januari hasa wakati huu ambako majumba yanatumia gesi kwa kiasi kikubwa kuwasha mifumo ya kupasha joto wakati huu wa majira ya baridi, inamaanisha Urusi, kuacha kutoa gesi kwa Ujerumani sio kitisho tena kwa taifa hilo.

Wakati Urusi ilipoivamia Ukraine miezi 11 iliyopita, Ujerumani ilikuwa inaagiza zaidi ya nusu ya gesi asilia kutoka Urusi. Kwahiyo kuihilibu Ujerumani lilikuwa jambo ambalo Moscow ilitumia kwa Umoja wa Ulaya ikiwa na nia ya kusambaratisha msaada Ukraine inaoupata kutoka Umoja huo.

Soma pia: Gesi ya Urusi yazidi kupungua kuingia Ulaya

Kwa sasa hivi Ujerumani iko katika mwezi wake wa tano, bila ya usaidizi wa kampuni ya nishati ya Gazprom kutoka Urusi na hii inamaanisha mpango wa Urusi umefeli. Wajerumani hawapigwi na baridi majumbani mwao na wala hawajalazimishwa kufunga makampuni yao. Wanasiasa mjini Berlin hawaogopi tena kwamba Urusi huenda ikataka kulipiza kisasi kwa Ujerumani kwa kuikwamisha nchi hiyo. Ujerumani yenyewe ilisitisha uagizaji wa nishati ya mkaa na mafuta ghafi kutoka Urusi kama sehemu ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa taifa hilo. Na Tangu mwishoni mwa mwezi Agosti haijaagiza gesi yoyote kutoka kampuni ya Gazprom nchini Urusi.

DW Journalist Andrey Gurkov
Andrey Gurkov wa DWPicha: DW

Kwa maneno mengine ni kwamba, Ujerumani haijaagiza gesi hiyo kutoka Urusi kwa miezi mitano sasa, na taifa hili lililo na uchumi mkubwa barani Ulaya linaonekana kufanya vizuri. Lakini kando na hilo  mgogoro wa kiuchumi bado unawapa wajerumani wasiwasi kutokana na kuporomoka kwa mfumo wa usambazaji wa nishati na kupanda kwa bei ya nishati hiyo muhimu ya gesi. Lakini utafiti unaonesha kuwa hilo huenda likatokea kwa asilimia ndogo.

Soma pia: Poland, Bulgaria zakatiwa gesi ya Urusi

Huku hayo yakiarifiwa Berlin inaendelea kutanua usaidizi wake kwa Kyiev jambo linaloonekana kama ushahidi wa moja kwa moja kwamba mipango ya Putin kuihilibu Ujerumani imefeli.  Mwanzoni mwa mwezi Januari wakati Ujerumani ilipokuwa inajaza hifadhi zake za gesi kwa wiki ya tatu mfululizo, serikali hiyo ilibadilisha msimamo wake na kuonekana kutoa msaada wa magari ya kivita kwa Ukraine huku harakati nyengine za kutoa vifaa zaidi zikifanyika na mjadala huo ukiendelezwa.

Kampuni ya nishati ya Urusi ya Gazprom imempoteza mteja wake mkubwa katika soko lake la nishati. Putin anaonekana kushindwa vibaya katika vita alivyodhamiria kuazisha vya gesi kati yake na mataifa ya Ulaya na hasa Ujerumani. Ujerumani imeuanza mwaka 2023 bila ya gesi kutoka Urusi na bila ya sababu ya aina yoyote ile ya wasiwasi juu ya gesi hiyo na hii ndio dalili kubwa ya kushindwa kwa Kremlin. Gesi asilia ya Urusi sio tena silaha yenye nguvu dhidi ya Ujerumani.

Kushindwa huku kuna  madhara makubwa zaidi kwa Uusi. Kampuni ya taifa ya nishati ya Gazprom imepoteza mauzo yake muhimu ya kigeni katika soko lake. Mwaka mmoja uliyopita robo ya mauazo yake yote yaliuzwa Ujerumani.

Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye Kijerumani