1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haitasimama kando

Admin.WagnerD27 Novemba 2015

Jeshi la Ujerumani litashiriki katika harakati za kupambana na magaidi wa "dola la kiislamu" ili kuonyesha mshikamano na Ufaransa baada ya mashambulio ya mjini Paris lakini haitasimama mstari wa mbele

https://p.dw.com/p/1HDO7
Ndege za Ujerumani zitafanya uplelezi dhidi ya magaidi
Ndege za Ujerumani zitafanya uplelezi dhidi ya magaidiPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Mashambulio yaliyofanywa na magaidi mjini Paris yamebadilisha kila kitu. Mashambulio hayo yamelichoma roho bara la Ulaya na sasa Ulaya inajibu mashambulio.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema bungeni kwamba juhudi za kupambana na magaidi wa "dola la kiislamu" zitaweza kufanikiwa kwa njia za kijeshi .Inapasa kuitilia maanani kauli hiyo.

Mpaka sasa Ujerumani imekuwa inaupiga chenga uamuzi wa kushiriki moja kwa moja katika harakati za kijeshi dhidi ya magaidi wa "dola la kiislamu." Badala yake Ujerumani imekuwa inawaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi wa kaskazini mwa Irak-Peshmerga. Labda ni mchango wa manufaa, lakini tangu kutokea mashambulio ya mjini Paris, Ujerumani haiwezi tena kujiweka nyuma na kujificha.

Ujerumani yakubali maombi ya Ufaransa

Mabadiliko yaliyofanywa na Ujerumani yametokana pia na maombi ya Ufaransa. Rais Hollande ameiomba Ujerumani ichukue hatua ndefu zaidi katika juhudi za kupambana na ugaidi. Na Kansela Merkel ameyaitikia maombi ya Ufaransa mara moja. Merkel ameonyesha mshikamano wa dhati na marafiki wa Ufaransa waliokumbwa vibaya na maafa ya ugaidi.

Mwandishi wa maoni Nina Werkhäuser
Mwandishi wa maoni Nina Werkhäuser

Jee Ujerumani inasisitiza kwamba,katika nyakati za migogoro,kwamba haitajikunyata na kusimama kando? Jeshi la Ujerumani litatoa mchango wake katika harakati za kupambana na magaidi . Na kwa hakika Ujerumani inapasa kuwa na msimamo huo ili kuonyesha kwamba ni nchi inayoweza kuaminika. Lakini pia ni uamuzi wa kushangaza.

Mpaka sasa imekuwa inaonekana kana kwamba, Ujerumani ililipata suluhisho jingine kwa kupanga kuliongeza jukumu lake nchini Mali ili kujiweka mbali na harakati za kupambana na magaidi wa "dola la kiislamu" nchini Syria!

Serikali ya Ujerumani haraka sana imeamua kuupitisha mpango kamambe wa kuziunga mkono harakati za kijeshi za kupambana na "Daesh" kama magaidi hao wanavyoitwa wakati mwingine.

Ujerumani itaoa ndege chapa ya Tornado zitakazotumika kwa ajili ya kufanyia upelelezi na pia itatoa meli za kuilinda manowari ya Ufaransa ya kubebea ndege na itasaidia katika kuzijaza mafuta ndege za Ufaransa angani.

Kwa hatua hizo Ujerumani inayatimiza matarajio za washirika wake.Hata hivyo askari wake hawatakuwamo katika mstari wa mbele wa mapambano.Itashiriki katika upelelezi,ugavi na usafirishaji lakini siyo haitapeleka askari wa miguu na wala ndege zake hazitashiriki katika kuzishambulia ngome za magaidi wa dola la kiislamu.

Lakini hapa pana kitendawili kwa Ujerumani. Bila ya nguvu za kijeshi haitawezekana kuwatokomeza magaidi .Na katika upande mwingine, kwa kadri nchi yoyote inavyojihusisha na harakati za kijeshi dhidi ya magaidi ndivyo hatari ya kushambuliwa na magaidi nayo inavyozidi kuwa kubwa, pia kwa Ujerumani.

Mwandishi:Werkhäuser Nina

Mfasiri:Mtullya Abdu.

Mhariri:Josephat Charo