Maoni ya wachambuzi leo yanalenga mustakabali wa Burundi baada ya kufanyika uchaguzi wa rais. Rais mteule Evariste Ndayishimiye alipata zaidi ya asilimia 50 ya kura na hivyo hapatahitajika kufanyika duru ya pili ya uchaguzi. Lakini upinzani umewasilisha kesi mahakamani ukidai uchaguzi uligubikwa na visa vya udanganyifu. Je hali itakuwa vipi?
Tega sikio usikie uchambuzi mbele ya Meza ya Duara