Maonesho ya utalii (ITB)-safari zapungua ?
11 Machi 2009Uchambuzi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umegusia mada mbali mbali tangu za ndani hata nje ya nchi: Miongoni mwa mada za nje ni kuripuka tena kwa machafuko katika Ireland ya kaskazini kati ya wakatoliki na waprotestanti.Nchini wahariri wamechambua msukosuko wa kisiasa anaopata wakati huu chamani Kanzela Angela Merkel lakini pia maonesho makubwa kabisa ya utalii ulimwenguni-ITB yanayofunguliwa rasmi leo mjini Berlin ni mada nyengine iliochambuliwa na wahariri hao.
Gazeti la Coburger Tageblatt juu ya ITB laandika:
"Utayarifu wa watalii kukata tiketi zao kwa safari za kitalii upo,lakini wingu kubwa mno lililotanda kwa wale wenye shakashaka lingali likiwazuwia baadhi.Si ajabu kutokana na taarifa mbaya kuwa biasharana nchi za nje inaanguka na wanojidai mabingwa wanashindana kutoa taarifa za kukatisha tamaa juu ya hali ya uchumi itakavyopkua.Kwa hali ya uchumi ilivyo,kuanguka kwa bidhaa zinazouzwa ngambo si jambo la kusangaza.
Ripoti kutoka viwanda vya magari na vya uundaji mashini,vimefanya hali kama hiyo kutarajiwa....Ndio, hali ya uchumi inatisha,lakini sio kusema Ujerumani iko ukingoni mwa kuporomoka hata ikiwa baadhi ya sauti zinazosikika zatoa dhana kma hiyo.
Likiendeleza mada hii ya ufunguzi wa leo wa maonesho makuu ya Utalii huko Berlin, gazeti la Nordwest-Zeitung laandika:
"Idadi ya aniria wa ndege na nchi zinazojitembeza kiutalii katika maonesho haya inapungua.Msdukosuko wa kuzorota uchumi unasababisha wasi wasi.Baadhi ya mashirika ya utalii kati kati ya msukosuko huu wa uchumi yaliotoa bei nafu kwa wanaokata tiketi na mapema na nafuu ambayo ilikua imalizike Februari au Machi,walirefusha muda.Mashirika mengine yameshusha hata bei.
hatahivyo, katika sekta nyengine biashara imepanda.Mfano katika safari za kitalii kwa meli,safari zinazojumuisha kila kitu katika bei na hata kwa safari za utalii nchini. Msukosuko wa fedha kwahivyo, unatoa fursa nzuri kwa utalii mikoani na mikoa inajua vipi kuitumia."
kuhusu dharuba ya kisiasa inayovuma usoni mwa Kanzela Angela Merkel wakati huu, gazeti la BILD Zeitung laandika:
"Bibi Angela Merkel , hayumbishwi tangu binafsi hata siasa zake.Yamkini lakini, taarifa za hali ya uchumi hazifurahishi,hatahivyo, Kanzela Merkel haoneshi kufadhahika na katulia baridi kabisa. Kwa hali hiyo, chamani kunatokota -chama chake cha CDU kinamtaka Kanzela Merkel kushika usukani na kutamba.Na bibi Merkel sio tu hawajibu wanaomkosoa, bali ananyosha tu njia yake ile ile.Kwani, wananchi wanamthamini kwa tabia yake hiyo nyakati za misukosuko...."
Gazeti la jiji la Cologne-Kolner-Stadt-Anzeiger linazungumzia kitisho cha kuchafuka upya mgogoro wa Ireland ya kaskazini baada ya kutulia kwa muda mrefu:Lauliza :
" Kuuliwa wanajeshi 2 wa kingereza na polisi mmoja huko .... kunaliamsha jiinamizi la kipindi cha kiasi miaka 30 cha hali ya hatari.Juu ya hivyo, hali haitarudi ilivyokua huko Ireland ya kaskazini.Hali mbaya ya kiuchumi kusini mwa mpaka,inawasadikisha hata wafuasi wa Jamhuri-"republicans" kuahirisha ndoto yao ya kukiunganisha tena kisiwa cha Ireland. Mbali na hayo, matamanio ya watu huko kuishi kwa amani na utulivu,ni makubwa mno."