1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiLibya

Manusura wa mafuriko Libya wakabiliwa na uhaba wa maji safi

18 Septemba 2023

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kuwa idadi ya vifo baada ya mafuriko nchini Libya imefikia watu 11,300.

https://p.dw.com/p/4WSeI
Mafuriko yamechanganya maji taka na safi
Mafuriko yamechanganya maji taka na safiPicha: Hamza Turkia/Xinhua/IMAGO

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu  ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kuwa idadi ya vifo baada ya mafuriko nchini Libya imefikia watu 11,300, lakini inahofiwa kuwa idadi kamili inaweza kuongezeka zaidi ya hapo.

Msemaji wa OCHA, Eri Kaneko, amesema ni vigumu kupata takwimu kamili za wahanga wakati zoezi la uokozi likiendelea.

Hadi sasa, Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha vifo 3,922, wakati wizara ya afya ya serikali ya mashariki mwa Libya ikisema kuwa watu 3,283 walikufa kufuatia mafuriko hayo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 1, 000 tayari wamezikwa katika makaburi ya jumla.

Watu ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko ya wiki iliyopita katika mji wa mashariki mwa Libya wa Derna, wanakabiliwa na mtanziko wa iwapo wabaki katika maeneo yao yaliyoharibiwa na kuwa hatarini kuambukizwa maradhi ya mripuko au kuondoka na kupita maeneo hatari ambako mabomu ya kutegwa ardhini yametawanywa na mafuriko hayo.

Mamlaka za Libya zimethibitisha kuwa watu 150  wameathiriwa kwa kutumia maji machafu.