Manusura bado wanaendelea kupatikana Uturuki na Syria
16 Februari 2023Jana Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 42 aliokolewa akiwa hai katika mkoa wa Kahramanmaras, baada ya kukaa chini ya kifusi kwa masaa 222.
Timu ya uokozi kutoka Uholanzi pia ilitangaza uokozi wa mafanikio wa watu wanne, wakiwemo wanaume watatu na mtoto, katika mji wa Antakya.
Wakati huo huo, serikali ya Uturuki imesema itavunja majengo yalioharibiwavibaya na kuanza ujenzi mpya.
Maafisa wanasema zaidi ya majengo 50,000 yameporomoka au kupata uharibifu mkubwa wakati wa matetemeko.
Soma pia:Uturuki yaahidi ujenzi mpya wa haraka baada ya tetemeko la ardhi
Katika mkoa wa kusini wa Hatay, nusu ya majengo yaliporomoka au yaliharibiwa vibaya kiasi kwamba yanapaswa kuvunjwa kabisaa.
Idadi jumla ya vifo nchini Uturuki na Syria imepanda hadi zaidi ya 41,000, na mamilioni wanahitaji msaada wa kiutu.
Maelfu yafamilia zimeachwa bila makazi, na zinapambana kuishi licha ya hali ya baridi kali.