1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANNHEIM : Aliekanusha maangamizi ya Wayahudi kifungoni

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRp

Mahkama ya Ujerumani imemhukumu Ernst Zuendel anayekanusha kutokea kwa Maangamizi ya Wayahudi kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kuchochea chuki za kikabila hiyo ikiwa ni adhabu ya juu kabisa inayoweza kutolewa kwa kosa hilo kwa mujibu wa sheria ya Ujerumani.

Mahkama katika mji wa kusini magharibi wa Mannheim wamemuona Zuendel kuwa na hatia kutokana na kurudia kukanusha mara kadhaa kutokea kwa mauaji ya Wayahudi milioni sita ambao waliuwawa na Manazi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Zuendel mwenye umri wa miaka 67 pia amesaidia kusambaza fasihi mbali mbali za chuki dhidi ya Wayahudi.Alirudishwa Ujerumani hapo mwaka 2005 kutoka Canada ambako alikuwa akiishi kwa miongo kadhaa.

Serikali ya Ujerumani inajaribu kuzirai nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zikubali kukanusha kutokea kwa Maangamizi ya Wayahudi kuwa kosa la jinai.