MANILA:Mkutano wa kilele wa ASEAN wafutwa
9 Desemba 2006Matangazo
Mkutano wa kilele wa nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEAN umefutiliwa mbali.
Mkutano huo wa viongozi wa eneo hilo ulitarajiwa kuanza hapo kesho katika kisiwa cha Cebu nchini Ufilipino.
Kumekuwepo na ati ati juu ya sababu za kufutwa kwa mkutano huo.Serikali ya Ufilipino imesema onyo la kutokea mvua kubwa katika eneo hilo limesababisha kuhairihswa kwa mkutano huo hadi januari.Awali Marekani pamoja na Australia zilionya kwamba kuna uwezekano wa kutokea mashambulio ya kigaidi dhidi ya mkutano huo.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Australia ilitoa ushauri kwa wasafiri wanaoelekea Ufilipino ikisema taarifa za karibuni zinafahamisha kwamba mipango ya kuandaa mashambulio ya kigaidi kwenye kisiwa cha Cebu imekamilika.