Man City wabeba Kombe la Dunia la Vilabu
23 Desemba 2023Manchester City imeshinda Kombe la Dunia la Vilabu kwa mara ya kwanza na kuhitimisha mwaka wa 2023 na mataji matano. City wamewacharaza Fluminense 4 - 0 mjini Jeddah Ijumaa usiku.
Soma pia: Manchester City hatimaye ni mabingwa wa Ulaya
Ushindi wa City umeendeleza utawala wa vilabu vya Ulaya kwenye mashindano hayo tangu mwaka wa 2012. Vilabu vya Ulaya vimeshinda mechi 22 mfululizo katika mashindano ya Kombe la Dunia la Vilabu.
Julian Alvarez aliifungia City bao la ufunguzi katika sekunde ya 45 kabla ya mchezaji wa Fluminense Nino kujifunga katika kipindi cha kwanza.
Phil Foden na Alvarez waligongelea msumari wa mwisho baadae katika kipindi cha pili. Baada ya kutwaa Champions League kwa mara ya kwanza na klabu hiyo, Premier League na Kombe la FA msimu uliopita, City pia walibeba UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza mwezi Agosti.