Dawa ya kikohozi yasitishwa Kenya baada ya wasiwasi wa sumu
12 Aprili 2024Hatua hii imechukuliwa siku moja baada ya Nigeria kutangaza hatua sawa na hiyo, ikisema dawa hiyo ina kiambata cha sumu.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Famisia na Sumu (PPB) nchini Kenya imesema imesitisha matumizi na kuamuru kurejeshwa kwa shehena fulani ya dawa ya kikohozi aina ya Benylin Paediatric.
Inafuatia tangazo la Nigeria kuwa vipimo vya maabara vimeonesha dawa hiyo ya maji ina kiwango cha juu cha kiambata kinachoamini kuwa sumu na inauhusishwa na vifo vya watoto kadhaa nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022. Vifo hivyo ni moja ya mikasa mibaya kabisa duniani iliyowahi kuhusishwa sumu kwenye dawa za kunywa na kumeza.
PPB imesema tayari imeanzisha uchunguzi na inafanya vipimo vyake vya maabara kuthibitisha vile vlivyofanywa na Nigeria. Shehena ya dawa inayolengwa ni ile iliyotengenezwa kampuni ya Johnson &Johnson tawi la Afrika Kusini mnamo mwezi Mei 2021 na kuwa muda wake wa mwisho wa matumizi wa Aprili 2024.