1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia waandamana kupinga uchimbaji haramu wa madini Kongo

8 Januari 2025

Mamia ya watu wameandamana katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kupinga uchimbaji haramu wa madini,mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4oxLe
Wachimbaji madini nchini Kongo
Wachimbaji madini nchini KongoPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Mamia ya watu wameandamana katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kupinga uchimbaji haramu wa madini,mashariki mwa nchi hiyo,ambako maafisa wanachunguza madai ya kusambaa kwa visa vya kuhusika kwa raia wa China kwenye shughuli hizo haramu.

Maandamano hayo yamefuatia tangazo la Jumapili la kukamatwa kwa raia watatu wa China waliokutwa na dhahabu pamoja na pesa nyingi taslimu, kwa mujibu wa gavana wa Kivu Kusini Jean Jacques Purusi.

Maafisa wa mkoa huo Mashariki mwa Kongo wenye utajiri  wa madini  wanasema mamia ya makampuni ya uchimbaji madini na hasa ya Wachina, yanachimba dhahabu bila ya kuonesha faida wanazopata kwa vyombo husika na mara nyingi shughuli hizo hufanywa bila ya vibali halali.