1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malkia Elizabeth mjini Berlin

Admin.WagnerD25 Juni 2015

Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza na mumewe Philip, leo wanaendelea kuutembelea mji mkuu wa Berlin. Wameshakutana na rais wa Ujerumani Gauck pamoja na kansela Merkel, na kushangiriwa na mamia ya wanafunzi wa shule.

https://p.dw.com/p/1Fn8F
Deutschland Schloss Bellevue Queen Merkel Staatsbankett
Malkia Elizabeth wa Uingereza na mumewe Philip, wakiwa na kansela wa Ujerumani Merkel katika kasri la BellevuePicha: Reuters/W. Kumm/Pool

Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili na mumewe Philip, wakiwa katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Ujerumani, wameanza siku yao ya pili leo hii mjini Berlin kwa kukutana na rais wa Ujerumani Joachim Gauck na mpenzi wake Daniela Schadt katika kasri lao la Bellevue.

Wakiwa katika kasri hilo, Malkia Elizabeth na mumewe walitia saini katika daftari la wageni kabla ya kutoka nje ya kasri hilo na kukutana na viongozi wangine.

Akiwa katika viwanja vya kasri la Bellevue, Malkia Elizabeth alikaribishwa kwa gwaride la jeshi lililomuimbia wimbo wa malkia wa Uingereza wa "Mungu mnusuru malkia" pamoja na wimbo wa taifa wa Ujerumani.

Deutschland Queen in Berlin weiße Mäuse
Msafara wa Malkia ukimshindikiza katika lango la BrandenburgPicha: Reuters/W. Rattay

Baadae walifanya safari fupi ya boti katika mto wa Spree, ambapo walishangiriwa na wanafunzi wa shule waliosimama katika daraja zilizo pembezoni mwa mto huku wakiwa wanapeperusha bendera za Uingereza na Ujerumani.

Malkia Elizabeth na mumewe Philip walikutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika ofisi yake na kuwajuulisha na mkuu wa wafanyakazi wa ofisi hio Peter Altmaier na kumpa ziara ya ofisi. Baadae Malkia huyo na mumewe walipanda gari lao na kuendelea na ziara yao ya mji mkuu huo wa Berlin.

Malkia Elizabeth atembelea jengo la kumbukumbu la waliokufa katika vita

Malika Elizabeth pia ametembelea jengo la kumbukumbu la waliokufa katika vita vya pili dunia la Neue Wache, na kuweka shada la mauwa kama ishara ya kuwakumbuka wahanga wote waliokufa wakati wa vita.

Deutschland Queen in Berlin Kranzniederlegung
Malkia Elizabeth atembelea jengo la kumbukumbu la waliokufa katika vitaPicha: Getty Images/AFP/A. Berry

Kesho malkia na mumewe watakuwa katika mji wa kibiashara wa Frankfurt, na muda maalum umetegwa wa kukutana na wakaazi katika uwanja mkuu wa mji huwo.

Na siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya mwisho ya ziara hio ya siku tatu, malkia Elizabeth na mumewe Philip watarudi tena Berlin na kukutana na wakaazi wa mji huo katika uwanja wa Pariser Platz kabla ya kutembelea iliyokuwa kambi ya mateso ya wanazi ya Bergen-Belsen, ambayo ilikombolewa na jeshi la Uingereza kutoka kwa wanazi tarehe 15 Aprili mwaka 1945 wakati wa kumalizika vita vya pili vya dunia. Aidha atakukutana na manusura na wanajeshi waliosaidia kuikomboa kambi hiyo.

Ingawa zaira hii ya malkia Elizabeth sio ya kisiasa, wachambuzi wakijerumani wanasema wakati uliyofanyika ziara hii unatoa ishara ya kisiasa. Ikiwa ni kipindi ambapo Uingereza inahitaji ungwaji mkono wa Ujerumani kuhusu mageuzi yanayoidaiwa na Uingereza ndani ya Umoja wa Ulaya.

Hii ni ziara rasmi ya tano kwa malkia Elizabeth wa pili na mumewe Philip, mara ya mwisho ikiwa mwaka 2004.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman