Mali yashindwa kulipa madeni yake
14 Februari 2022Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa fedha wa Afrika Magharibi.
Tangu mwezi wa Januari, wakala unaoshughulikia madeni wa ukanda huo, Umoa-Titres, umechapisha kwa wawekezaji kuashiria kwamba Mali haijakuwa ikilipa madeni yake katika soko la mitaji ya kifedha la umma kufikia kima cha faranga bilioni 53 sawa na euro bilioni 81, chapisho la mwisho likitolewa Ijumaa iliyopita.
Mnamo Februari 2, Mali ilitangaza imeshindwa kulipa malipo yake kuhusiana na mikopo miwili ya hati za dhamana kufikia jumla ya faranga bilioni 2.6 kutokana na vikwazo.
Januari mwaka huu, jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, iliiwekea vikwazo Mali kujibu hatua ya utawala wa kijeshi kuahirisha uchaguzi ulioahidi tangu 2020 wakati ulipotwaa madaraka, ambayo iliungwa mkono na Ufaransa, Marekani na Umoja wa Ulaya.