1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalaysia

Malaysia yalenga kuboresha ushirikiano wa ASEAN

19 Januari 2025

Mawaziri wa mambo ya nje Mataifa ya Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, wamefanya mkutano wa faragha nchini Malaysia.

https://p.dw.com/p/4pLNM
Mkutano wa ASEAN
Malaysia yalenga kuboresha ushirikiano wa jumuiya ya ASEANPicha: Yasuyoshi Chiba/REUTERS

Malaysia imeandaa mkutano huo kwa mara ya kwanza kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo huku kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoongezeka nchini Myanmar na mivutano  katika Bahari ya Kusini ya China.

Soma pia: ASEAN; Myanmar haipaswi kufikiria uchaguzi kwa sasa

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Malaysia Amran Mohamed Zin, amesema wamejitolea sio tu katika kushughulikia masuala ya kikanda lakini pia mgogoro wa  Myanmar na k

uendelezwa  mazungumzo juu ya Kanuni za maadili za Jumuiya ya ASEAN na China kuhusu eneo la Bahari ya Kusini mwa China.

Wakimbizi wa Rohingya waelezea hali mbaya ya ghasia Myanmar