Malawi: Mahakama yatupilia mbali ombi la Mutharika
13 Februari 2020Matangazo
Jaji Dingiswayo Madise amesema hiyo ilikuwa ni kesi ya sheria ya umma na lazima sheria ifuatwe kwa umakini. Mahakama hiyo pia iliikataa hoja ya tume ya uchaguzi kuwa uchaguzi mwingine utakuwa ni gharama kubwa kwa taifa hilo maskini. Jaji Madise amesema demokrasia ina gharama kubwa. Haki za raia ni muhimu na kwa hiyo mahakama haitozuia kufanyika kwa uchaguzi halali unaokubalika kikatiba kwa kusingzia gharama. Mahakama hiyo iliyabatilisha matokeo ambayo yalimpa Mutharika ushindi mwembamba, ikitaja matukio mengi ya dosari na udanganyifu. Iliamuru nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika kuandaa uchaguzi mpya katika kipindi cha siku 150 na uchunguzi katika operesheni za tume ya uchaguzi.