Tunisia yatakiwa kuimarisha uhuru wa kujieleza
18 Mei 2024Matangazo
Mashirika hayo pia yamesema utawala unatumia mahakama na polisi kuwaadhibu wapinzani wao.
Mwezi huu pekee polisi iliwakamata watu 10 wakiwemo mawakili, wanaharakati, waandishi habari, na maafisa wa mashirika ya kiraia katika kile Amnesty Internationa na Human Rights Watch ilichokielezea kama kamata kamata dhidi ya wapinzani wa serikali.
Amri dhidi ya "habari za uongo" inawakandamiza wakosoaji,Tunisia
Mashirika hayo yametoa wito kwa serikali ya Saied kuheshimu haki ya uhuru wa kujieleza ya watu wa Tunisia