Wapigania haki wamsihi rais wa IOC kuondoa marufuku ya hijab
12 Juni 2024Vyama vya michezo na makundi ya haki za binadamu yametoa wito kwa rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach kusaidia kubatilisha marufuku ya wanamichezo wa Ufaransa kuvaa hijab, wakisema kuwa inadhoofisha maadhimisho ya mwanzo ya Olimpiki ya usawa wa kijinsia.Wakati IOC mwezi Septemba ilipotangaza kwamba wanamichezo wanaoshiriki katika Michezo ya Paris wataruhusiwa kuvaa hijab, Waziri wa Michezo wa Ufaransa Amelie Oudea-Castera aliwazuia wanariadha wa Ufaransa kufanya hivyo, akisema wanafungwa na mgawanyiko mkali wa nchi wa kidini. Shirika la Amnesty International na makundi mengine 10 yaliotia saini barua ya Mei 24 kwa Bach, yanasema marufuku hiyo ni kinyume na Mkataba wa Olimpiki na ni sehemu ya suala kubwa kuhusu ubaguzi dhidi ya wanamichezo wa wa kike wa Kiislamu katika ngazi zote za nchini Ufaransa. Marufuku ya hijabu imesababisha ubaguzi, udhalilishaji dhidi ya wanamichezo Waislamu nchini Ufaransa, ambao baadhi yao wameondoka nchini humo kutafuta fursa mahali pengine.