1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makumi ya wanachama wa Ennahda wakamatwa Tunisia

14 Septemba 2024

Wanachama kadhaa wa chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Tunisia, cha Ennahda, wamekatwa wiki hii kuelekea kuanza rasmi wikendi hii kwa msimu wa kampeni za uchaguzi wa rais.

https://p.dw.com/p/4kcW5
Tunisi, Tunisia | Maandamno dhidi ya rais Kais Saied.
Ndugu wakiwa na picha za wapendwa wao waliokamatwa TunisiaPicha: Chokri Mahjoub/ZUMA Press Wire/picture alliance

Waziri wa zamani wa vijana na michezo Ahmed Gaaloul, mwanachama wa kamati kuu ya chama hicho, na mshauri wa kiongozi wa chama aliefungwa Rached Ghannouchi, amesema chama kimehisabu watu wasiopungua 80 waliokamatwa, na kilikuwa kwenye mchakato wa kuhakiki jumla ya wasiopungua 108.

Katika taarifa, chama cha Ennahda kimeitaja kamatakamata hiyo kuwa kampeni isiyokifani ya uvamizi na ukiukaji wa haki za msingi zaidi zinazohakikishwa na sheria.

Kamatakamata ya Ijumaa ilihusisha maafisa wa ngazi ya juu wa chama, akiwemo Mohamed Guelwi, mjumbe wa kamati kuu, na Mohamed Ali Boukhatim, kiongozi wa chama wa mkoa kutoka kiunga cha Tunis.