1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya serikali mpya yasainiwa Ujerumani

12 Machi 2018

Viongozi wa vyama na makundi ya wabunge kutoka vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU na wenzao wa SPD walitia saini Ijumaa mjini Berlin, makubaliano yaliyofikiwa mapema mwezi uliopita wa Februari.

https://p.dw.com/p/2uBts
Deutschland Unterzeichnung Koalitionsvertrag
Picha: picture-alliance/dpa/AP Photo/M. Schreiber

Makubaliano hayo yalikuwa kuhusu kuundwa serikali mpya ya muungano-GroKo.

Takriban miezi sita baada ya uchaguzi mkuu, viongozi wa vyama vya CDU/CSU na SPD wametia saini makubaliano ya kuunda serikali mpya. Hatimae  ikawa zamu ya mwenyekiti wa CDU, Angela Merkel, CSU Horst Seehofer na kaimu mwenyekiti wa SPD Olaf Scholz kukutana na kutia saini makaubaliano hayo ya kurasa 177.

Jumatano inayokuja Kansela Angela Merkel atachaguliwa na bunge kuendelea na muhula wake wa nne madarakani na baadae baraza jipya la mawaziiri litaapishwa.

Serikali ihakikishe mshikamano katika jamii

Mkataba wa kuunda serikali ya muungano wa vyama vikuu una uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizoko hivi sasa, unashauri njia za kuzipatia ufumbuzi na kupendekeza namna ya kuimarisha hali ya maisha ya waanchi" amesema kansela Merkel alipokuwa akitia saini mkataba huo."Kazi nyingi ,na ngumu zinatusubiri" amesisitiza kansela na kusema "ni kazi ya furaha ."

Deutschland Unterzeichnung Koalitionsvertrag
Viongozi wa vyama vilivyounda serikali ya muungano Ujerumani wakitia saini mkatabaPicha: picture-alliance/dpa/AA/E. Basay

Serikali ya muungano wa vyama vikuu inabidi ihakikishe mshikamano katika jamii" alisema kaimu mwenyekiti wa SPD Olaf Scholz. "Tunabidi kila siku kuwajibika na kuanzia sasa kutekeleza yaliyomo katika mkataba wa kuunmda serikali ya muungano" amesema.

Mwenyekiti wa CSU, Horst Seehofer aliutaja mkataba huo kuwa "ni muongozo wa maana" unaoweka uzani sawa kati ya vyama vitatu vikuu. Kwa maoni yake makubaliano yaliyofikiwa ni kwa masilahi ya raia wa kawaida:"Wao ndio tabaka ya kati ya jamii". Sasa serikali inabidi iharakishe, alishadidia mwanasiasa huyo aliyeteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Viongozi hao watahakikisha hali bora ya maisha Ujerumani

Kabla ya  viongozi hao wa CDU, SPD na CSU, Merkel, Scholz na Seehofer, ili kuwa zamu ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Annegret Kramp-Karrenbauer wa CDU, Andreas Scheuer wa CSU na Lars Klingbeil wa SPD pamoja pia na mkuu wa kundi la wabunge wa vyama ndugu vya CDU/CSU Volker Kauder, mkuu wa kuindi la wabunge wa SPD Andrea Nahles na  Alexander Dobrindt wa wabunge wa  CSU katika jimbo la kusini la Bavaria, kutia saini makubaliano hayo.

Deutschland Unterzeichnung Koalitionsvertrag
Kansela Angela Merkel (katikati), Olaf Scholz (kushoto) na Horst Seehofer (kulia) Picha: picture-alliance/dpa/AA/E. Basay

Katika mkutano na waandishi habari viongozi wote watatu wamesisitiza watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hali bora ya maisha nchini Ujerumani. Wamesema pia watajitahidi kuwaondolea wananchi hofu walizo nazo kuelekea utandawazi na pia digitali. "Lengo la serikali mpya ni kuhakikisha neema katika enzi za utandawazi na digitali" alisema kansela Merkel.

Upande wa upinzani katika bunge la shirikisho Bundestag wamekosoa mkataba huo wa serikali mpya ya muungano.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/AFP

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman