1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maktaba kubwa zaidi Afrika Mashariki yazinduliwa Tanzania

​​​​​​​Anuary Mkama27 Novemba 2018

Rais John Magufuli amezindua maktaba ya kisasa ya mfumo wa teknolojia ya mawasiliano na ambayo inaelezwa kuwa kubwa zaidi Afrika mashariki.

https://p.dw.com/p/38zni
Symbolbild Universität Seminar Bibliothek Flirt
Picha: Yü Lan/Fotolia

Maktaba ya kisasa inayotumia  mfumo wa teknolojia ya mawasiliano ambayo inaelezwa ndio kubwa zaidi katika eneo la Afrika Mashariki pamoja kusini mwa Afrika,imefunguliwa leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Dkt John Magufuli. Mwandishi wetu kutoka Dar es Salaam Anuary Mkama amehudhuria ufunguzi huo na ametuandalia taarifa ifuatayo.

Katika hotuba yake  kwenye ufunguzi wa maktaba hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa China, Rais Magufuli amesema maktaba hiyo ni nyumba ya maarifa hivyo itasaidia kuinua kiwango cha elimu pamoja na maendeleo katika sekta nyingine kupitia utafiti.

Rais Magufuli na Edward Lowassa wakati wa uzinduzi wa maktaba katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Magufuli na Edward Lowassa wakati wa uzinduzi wa maktaba katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.Picha: DW/S. Khamis

Mapema, makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof William Anangisye ameelezea uwezo wa maktaba hiyo katika kuwahudumia wanafunzi.

Nao wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamekiri kufurahishwa na ujenzi wa maktaba hiyo

Kwa mujibu wa balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Wang Ke, nchi yake imetumia kiasi cha dola za kimarekani million 41 kujenga maktaba hiyo ya kisasa pamoja na kituo cha kufundishia lugha ya kichina.

Katika tukio lisilotegemewa Rais Dkt Magufuli alimpongeza Waziri Mkuu  wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa ni mmoja wa wageni katika hafla hiyo kwa kumtaja kuwa ni mwanasiasa aliyekomaa lakini akitoa onyo kwa wanasiasa wanaovunja sheria.

Rais Magufuli na Edward Lowassa wakinong'ona wakati wa uzinduzi wa maktaba kubwa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Magufuli na Edward Lowassa wakinong'ona wakati wa uzinduzi wa maktaba kubwa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.Picha: DW/S. Khamis

Baada ya kukaribisha na  Rais Magufuli, Lowassa  aliyekuwa mgombea urais wa ushirika wa vyama vya chadema, cuf, Nccr mageuzi na NLD maarufu kama UKAWA wakati wa uchaguzi wa 2015 , alipongeza juhudi zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na serikali  katika kuimarisha elimu.

Ujenzi wa maktaba hio ni mradi wa pili mkubwa kufadhiliwa na China nchini Tanzania, baada ya ule wa reli ya Tazara, kutoka Tanzania hadi Zambia iliofunguliwa 1975.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman