1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makombora ya Urusi yauwa 6 Odessa

10 Oktoba 2024

Watu sita wameuawa kwa mashambulizi ya anga ya Urusi kwenye mji wa bandari ya kusini mwa Ukraine, Odessa.

https://p.dw.com/p/4lbXt
Wakimbizi, Romania, Ukraine
Meli yenye wakimbizi ikitokea Odessa kuingia mpaka wa Romania.Picha: Alessandro Serrano/Avalon/Photoshot/picture alliance

Kwa mujibu wa gavana wa kijeshi wa mkoa huo, Oleh Kiper, watu wengine 11 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya jana.

Gavana huyo ameongeza pia kwamba meli ya mizigo inayopeperusha bendera ya Panama nayo pia ilishambuliwa.

Haya ni mashambulizi ya tatu dhidi ya meli ya kiraia ndani ya kipindi cha siku nne, kwa mujibu wa gavana huyo.

Soma zaidi: Mkutano wa kilele kuhusu Ukraine huko Ramstein waahirishwa

Urusi imekuwa ikijaribu kuizuwia njia ya kupitishia nafaka iliyoanzishwa na Ukraine, baada ya kuzifungia bandari zote mwanzoni mwa vita vyake zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Lakini baadaye, kutokana na umuhimu wa nafaka za Ukraine kwenye soko la dunia, nchi zote mbili zilikubaliana kuanzia ujia maalum na kwa kipindi maalum, ambacho kilimazika mwezi Juni 2023..

Tangu hapo, Ukraine imekuwa ikitumia njia zake yenyewe baada ya kuzifurusha meli za kijeshi za Urusi kutoka eneo la magharibi mwa Bahari Nyeusi.