Licha ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo sehemu kubwa ya ardhi yake imezungukwa na miti, iko katika hatari ya kutoweka, ikiwa suluhu za nishati safi na endelevu hazitapewa kipaumbele ili kuwasaidia wananchi hasa wa vijijini kuachana na matumizi ya mkaa na kuni. Tunaangazia hilo kwa undani kwenye makala ya 'Mtu na Mazingira'. Msimulizi ni Salma Mkalibala.