Mahasimu katika vita vya Yemen wabadilishana wafungwa
15 Aprili 2023Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imearifu leo kuwa mamia ya wafungwa wa kivita, wakiwemo raia wa Saudi Arabia, wameachiwa leo katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa baina ya serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia, na kundi la waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.
Wafungwa karibu 900 wamesafirishwa kwa ndege kati ya Saudi Arabia na maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi, wakati matumaini ya kumalizika kwa vita vya miaka minane nchini Yemen yakiongezeka.
Ndege ya kwanza imeondoka katika mji wa Abha wa kusini mwa Saudi Arabia ikibeba wafungwa 120 wa Kihouthi, ikiwa ni kwa mujibu wa afisa wa mahusiano wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Jessica Moussan.
Ndege nyingine imeondoka mjini Sanaa, ikiwa na wafungwa 20, 16 miongoni mwao wakiwa raia wa Saudi Arabia, na watatu wakiwa Wasudan.
Chanzo: AFPE