Mahakama yaruhusu udukuzi wa simu Munich
10 Agosti 2024Ofisi ya Muendesha Mashitaka mjini Munich inawachunguza wanaharakati hao inaowatuhumu kuunda kundi la kihalifu.
Lakini waandishi wa habari walikuwa wamefungua kesi kupinga uamuzi wa mahakama moja ya wilaya kuruhusu kufuatiliwa kwa simu zao.
Soma zaidi: Kizazi cha mwisho waitisha maandamano ya tabianchi Ujerumani
Mahakama ya jimbo mjini Munich imesema kesi hiyo haina msingi, kwa hoja kwamba mazungumzo ya simu yanayobishaniwa hayakuwa ni kwa ajili ya waandishi wa habari pekee.
Kwa mujibu wa majalada ya kesi hiyo, polisi inalishuku kundi la Last Generation kwa kuwa na tabia za kihalifu.
Mahakama imesema kwenye mazingira kama hayo, polisi ina haki kisheria kutegesha mazungumzo ya simu.
Wanaharakati wa kundi hilo wamekuwa wakifanya maandamano kwenye viwanja vya ndege na barabara kuu, kupinga uchafuzi wa mazingira.