Mahakama yabatilisha kifungo cha mtoto wa Santos wa Angola
5 Aprili 2024Majaji wa mahakama hiyo ya juu katika mji mkuu wa Luanda walitangaza siku ya Alkhamis (Aprili 4) kwamba hukumu iliyotolewa mwaka 2020 dhidi ya Jose Filomeno dos Santos ilikuwa batili na "kinyume cha katiba".
Filomeno dos Santos, mwenye umri wa miaka 46, amekuwa akitumikia hukumu yake kwa kifungo cha nyumbani baada ya kutiwa hatiani kwa kuiba dola milioni 500 kutoka hazina ya serikali ambayo aliisimamia kuanzia 2013 hadi 2018.
Soma zaidi: Binti wa rais wa zamani wa Angola anakanusha madai ya ufisadi
Hata hivyo haijabainika iwapo mtoto huyo wa marehemu Eduardo dos Santos aliyepewa jina la utani "Zenu" ataachiwa huru au atafunguliwa kesi mpya.
Zenu alikuwa mtu wa kwanza kwenye familia ya rais wa zamani kufunguliwa mashtaka kama sehemu ya kampeni ya kupinga ufisadi iliyoongozwa na Rais Joao Lourenco tangu alipoingia madarakani mnamo 2017.