Mahakama Uganda yamhukumu mwanachama wa IS miaka 10 jela
27 Agosti 2024Matangazo
Uganda imetoa hukumu ya kwenda jela miaka 10 kwa mwanachama mmoja wa kundi linalofungamanishwa na mtandao unaojiita dola la kiislamu.
Mtu huyo amehusishwa na tukio la njama ya jaribio la shambulio la kigaidi katika shughuli ya mazishi ya kamanda mmoja wa ngazi za juu wa jeshi la Uganda miaka mitatu iliyopita.
Soma: Kitisho cha tukio la ugaidi Uganda
Rashid Katumba alikamatwa mwaka 2021 akiwa na vifaa vya kuripuka katika mji wa kaskazini wa Pader siku ya mkesha wa shughuli ya mazishi ya jenerali Paul Lokech,aliyekuwa akifahamika zaidi kwa jina la Simba wa Mogadishu.
Kitengo cha kushughulikia uhalifu wa kimataifa katika mahakama ya Uganda kimemhukumu Katumbi pamoja na washtakiwa weengine wawili LuyenjeNajjimu na Arafat Jamil Kiyemba.