Sheria na Haki
Ufaransa yatoa waranti mpya wa kukamatwa kwa Bashar al-Assad
22 Januari 2025Matangazo
Chanzo kimoja kimesema hii ni hatua ya pili kama hiyo kuchukuliwa na mamlaka za haki za Ufaransa. Waranti huo wa kukamatwa umetolewa kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya mwalimu wa zamani raia wa Ufaransa aliyekuwa na uraia wa Syria na Ufaransa.
Salah Abou Nabout aliyekuwa na umri wa miaka 59, aliuwawa mnamo Juini 7 mwaka 2017 kufuatia kulipuliwa kwa nyumba yake na helikopta za jeshi la Syria.
Kulingana na chanzo kimoja, ídara ya mahakama ya Ufaransa inachukulia kwamba Assad ndiye aliyeamrisha na kufadhili kufanyika kwa shambulizi hilo.
Maafisa wengine sita waandamizi katika jeshi la Syria tayari wametolewa waranti wa kukamatwa kuhusiana na kesi hiyo katika uchunguzi ulioanza mwaka 2018.