1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kijeshi nchini DRC yawahukumu kifo askari 22

8 Julai 2024

Mahakama ya kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewahukumu kifo wanajeshi 22 kwa makosa ya kile kilichotajwa kuwa ni "kumkimbia adui" wakati wa mapigano na waasi wa M23.

https://p.dw.com/p/4i1eb
DR Kongo
Baadhi ya wanajeshi wa Kongo wakiwa mjini Goma Picha: Wang Guansen/Xinhua/picture alliance

Mawakili wamesema wanajeshi 16 walihukumiwa kifo katika kesi moja katika jimbo la Kivu Kaskazini, na wengine sita katika kesi tofauti, ambazo zinajiri siku chache baada ya wanajeshi wengine 25 kupewa hukumu sawa na hiyo.

Hukumu hizi zinatolewa wakati waasi wa M23 wakijiimarisha katika wiki za hivi karibuni kwa kuchukua udhibiti wa maeneo huko mashariki mwa Kongo. 

Wanajeshi wawili wahukumiwa kifo kwa uoga nchini Congo

Wataalam wa Umoja wa mataifa wamebainisha kuwa wanajeshi wa Rwanda wapatao 3000 hadi 4000 wanashirikiana na waasi wa M23, tuhuma ambazo zimekuwa mara kadhaa zikikanushwa na serikali mjini Kigali.